Monthly Medjugorje Messages
Languages:
English,
Afrikaans,
العربية,
Български,
Беларуская,
Català,
Čeština,
Deutsch,
Español,
Français,
Hrvatski,
Italiano,
Kiswahili,
Latviešu,
Magyar,
Malti,
Nederlands,
Norsk,
Polski,
Português,
Română,
Русский,
Shqip,
Slovenčina,
Slovenščina,
Suomi,
Svenska,
Tagalog,
Tiếng Việt,
Українська,
زبان_فارسی
“Wanangu wapendwa! Wakati huu uwe kwenu wakati wa maombi ya amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Wanangu, wapenzi wangu! Mmechaguliwa kwa sababu mmeitikia, mmeweka maelekezo yangu katika vitendo, na mnampenda Mungu zaidi ya yote. Kwa hiyo, wanangu, ombeni kwa moyo wote ili maneno yangu yapate kutimia. Fungeni, toeni sadaka, pendeni kwa upendo wa Mungu aliyewaumba, na muwe, wanangu, mikono yangu iliyonyooshwa kwa ulimwengu huu ambao haujapata kumjua Mungu wa upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ambao Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kwenye njia ya utakatifu, Shetani anataka kuwatia ninyi kwa kamba ya kutotulia na chuki. Msimruhusu ashinde, bali piganeni, wanangu, kwa ajili ya utakatifu wa kila maisha ya mwanadamu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Pia leo namshukuru Mwenyezi kwa kuwa pamoja nanyi na kuweza kuwaongoza kuelekea kwa Mungu wa upendo na amani. Itikadi zinazowabomoa ninyi na maisha yenu ya kiroho ni za mpito. Ninawaita ninyi wanangu, mrudieni Mungu kwa maana kwa Mungu mnayo wakati ujao na uzima wa milele. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika muwe watu wa matumaini, amani na furaha, ili kila mtu awe mtunza amani na mpenda maisha. Wanangu, ombeni kwa Roho Mtakatifu ili awajaze kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu za ujasiri na kuachwa. Wakati huu pia utakuwa zawadi kwenu na safari katika utakatifu kuelekea uzima wa milele. Niko pamoja nanyi na ninawapenda. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Upepo wa kutotulia, ubinafsi na dhambi huteka nyoyo nyingi na kuzipeleka kwenye kutotulia na kuangamia. Kwa hiyo, ninawaalika ninyi, wanangu, mrudi kwa Mungu na kusali ili mpate kuwa na afya njema mioyoni mwenu na katika nchi mnayoishi. Ninawapenda ninyi wanangu, na ndiyo maana sichoki kuwaalika mgeuke. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika mwaka huu wa neema ninawaalika kwenye uongofu. Wanangu wapendwa, mtangulizeni Mungu katika maisha yenu na matunda yake yatakuwa upendo kwa jirani na furaha ya kushuhudia; utakatifu wa maisha yenu utakuwa ushuhuda wa kweli wa imani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Ombeni, ombeni, ombeni ili amani itawale katika kila moyo na kushinda uovu na mahangaiko yote. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ya kusubiri, napenda kuwaalika kusali ili Majilio yawe ni maombi ya familia. Kwa namna ya pekee, wanangu, ambao ninawakumbatia kwa upole, nawasihi muombe amani duniani, ili amani ishinde juu ya mahangaiko na chuki. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu, mnapoadhimisha Siku ya Watakatifu Wote, waombeni maombezi na sala zao, ili kwa ushirika nao, mtapata amani. Watakatifu wawe waombezi kwenu na mifano ya kuigwa katika kuishi maisha matakatifu. Mimi nipo pamoja nanyi na ninawaombea kwa Mungu kwa kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Kwa kuwapenda ninyi, Mungu alinituma kati yenu ili kuwapenda ninyi na kuwasihi katika sala na uongofu, kwa ajili ya amani ndani yenu, katika familia zenu na katika dunia. Wanangu, msisahau kwamba amani ya kweli huja tu, kwa njia ya maombi, kutoka kwa Mungu ambaye ndiye amani yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Leo maombi yangu pamoja nanyi ni kwa ajili ya amani. Mema na maovu yanapigana na kutaka kutawala duniani na katika mioyo ya watu. Muwe watu wa matumaini, maombi na imani kubwa kwa Mungu Muumba ambaye kwake yote yanawezekana. Wanangu, amani na itawale ndani yenu na karibu nanyi. Ninawabariki kwa baraka yangu ya kimama ili, wanangu, muwe furaha kwa wale wote mtakaokutana nao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose